Marekani imeionya China kuhusu mpango wake wa kupeleka wanajeshi wake katika visiwa ilivyojenga baharini kusini mwa nchi hiyo kwaajili ya kujilinda na maadui wa taifa hilo.

Onyo hilo limetolewa na Waziri wa ulinzi wa Marekani, James Mattis katika mkutano wa kujadili masuala ya usalama uliofanyika Singapore, ambapo amesema kupeleka wanajeshi katika visiwa hivyo kutahatarisha amani ya dunia.

Aidha, ameongeza kuwa kama China itaendelea na mpango wake wa kupeleka wanajeshi katika visiwa hivyo, kuha hatari kubwa uhusiano kati ya nchi hizo kuvurugika na kuhatarisha amani ya eneo hilo.

Hata hivyo, hatua hiyo ya Marekani imekuja mara baada ya Baraza la Usalama kuiongezea vikwazo Korea ya Kaskazini kufuatia kufanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa marefhu.

Mwili wa mzee Francis Kanyasu 'Ngosha' waagwa Muhimbili
Watoto wafariki kwa chanjo ya surua isiyo salama