Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anakaribia kufanya usajili wake wa kwanza baada ya kinda wa Serbia Marko Grujic kuwasili Merseyside kwaajili ya vipimo vya afya.

Liverpool ilikubaliana na klabu ya Red Star Belgrade kabla ya Krisimas juu ya ada ya pauni milioni 5.1 kwaajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19.

Marko Grujic  akawasili England wikiendi iliyopita kwaajili ya kukamilisha dili lake la kujiunga na Liverpool.

Usajili wake unatarajiwa kutangazwa Jumanne, lakini kinda huyo atarejea Red Star kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu.

Chelsea Na Man Utd Zawania Saini Ya Beki Wa Kibrazil
Florentino Perez Aanika Sababbu Za Kumtimua Benitez