Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland Martin O’Neill amekanusha taarifa za kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Hull city inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England (PL).

O’Neill amekanusha uvumi huo alipohojiwa na vyombo vya habari mara baada ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Serbia uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo na timu hizo kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili.

“Sifikirii jambo lolote kuhusu uvumi huo,”

“Nipo hapa kwa makubaliano ya kimkataba na ninaheshimu suala hilo, kwa hiyo sitokua na mpango wa kufikiria kuondoka mpaka niweze kutimiza malengo niliyojiwekea katika timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland.” Alisema O’Neill.

Jina la O’Neill limekua likitajwa miongoni mwa majina ya mameneja ambao wanapewa kipaumbele cha kuchukua nafasi ya Steve Bruce aliyetangaza kujizulu miezi mitatu iliyopita.

Kwa sasa kikosi cha Hull City kinanolewa na meneja wa muda Mike Phelan ambaye ameonyesha kuwa na mtiririko mzuri wa matokeo tangu kuanza kwa msimu huu, kufuatia matokeo ya sare mbili na ushindi mara mmoja.

Video: Kama bado unatumia simu feki kwa matumizi mengine, Serikali imetoa maelezo haya
Video: Majibu ya Serikali kuhusu upungufu wa vifaa tiba na wataalamu hospitali za Jeshi