Uongozi wa Simba SC umesema rasmi umeingia chimbo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanarudisha makali ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ili waweze kutwaa mataji muhimu na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Simba SC msimu huu wameshindwa kufanya vyema mara baada ya kukosa ubingwa katika michuano yoyote ambayo wameshiriki huku kimataifa wakiishia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa tayari wameshaingia chimbo kwa ajili ya kuuandaa msimu mpya ambao watarejea kwa kishindo kwa ajili ya kuurudisha ufalme wao katika kichuano yote.

“Wanasimba naomba muwe watulivu sana wala msiyumbuishwe na maneno ya watu kwani nataka niwahakikishie kuwa tayari tumeshaingia chimbo kwa ajili ya kuirudisha Simba msimu ujao katika ufalme wake.

“Simba kwa msimu ujao lazima irudishe ule ufalme wake wa kuyatawala mataji yake yote ambayo tulikuwa tukiyamiliki bila kusahau michuano ya kimataifa, tunatambua msimu huu haujakuwa mzuri lakini kwa msimu ujao lazima tuwaonyeshe kuwa Simba,” amesema Ahmed Ally

Rio Ferdinand amchana Carlo Ancelotti
Marcus Rashford apandisha mzuka Man Utd