Mataifa mbalimbali Barani Afrika yatakuwa yakijiandaa kwa chaguzi mbalimbali ikiwemo nchi ya Benin ambayo wabunge watapigiwa kura hapo Januari 8, 2023 huku nchi nane zikikabiliwa na uchaguzi Mkuu wa nafasi ya urais.
Nchi kubwa barani Afrika yenye wakazi zaidi ya milioni 200 Taifa la Nigeria, lenye we litafanya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Februari 25, 2023kwa na baadaye mwezi Machi utafuata ule wa serikali za mitaa na magavana.
Taifa la Sierra Leone, nalo litafanya uchaguzi wa urais mwezi Juni 2023 huku Liberia yenyewe ikitaraji kumchagua uais mwezi Oktoba na Madagascar mwezi Novemba na viongozi wa mataifa hayo Julius Maada Bio, George Weah na Andry Rajoelina wanaomaliza muda wao wanaweza kugombea tena.
Huko Gabon, Katiba inamruhusu Rais Ali Bongo kugombea tena iwapo atataka na kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uchaguzi wa urais umepangwa rasmi kufanyika Desemba 20, 2023 huku Taifa la Zimbabwe nalo likitaraji kufanya uchaguzi mkuu ndani ya mwaka huu (2023).