Baraza la Mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika septemba 2023 ambapo watahiniwa milioni 1,073,402 kati ya 1,356,392 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamefaulu huku kiwango cha ufauli kikiongezaka kwa asilimia 0.96ikilinganishwa na mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katibu mtendaji NECTA Dkt. Said Mohamed amesema wanafunzi 31 wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kujihusisha na vitenda vya udanganyifu na kwamba vituo viwili vya mitihani Twibhoki na Graiyaki vyote vya mkoa wa Mara vimefungiwa baada ya kuthibitisha kupanga njama za kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

”Vituo hivyo vimethibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mtihani vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mtihani 2016 mpaka hapo Necta itakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya Taifa” amesema Dkt Mohamed.

Kwa upande wa ufaulu kwa ujumla amesema havijatofautiana sana kati ya wavulana na wasichana huku akieleza kupanda kwa ufauli katika somo la sayansi na teknolojia kwa asilimia 2.45 na kushuka kwa ufaulu katika somo la hisabati kwa asilimia 4.46.

”Ufaulu wa somo la hisabati umeshuka kutoka silimia 52 mwaka jana hadi asilimia 48.83 mwaka huu kwani asilimia 51 ya watahiniwa wote wamepata daraja ‘D” amebainisha.

GGML, CCBRT wakabidhi Vitimwendo kwa wenye Ulemavu
Mwanafunzi aliyefariki Israel mwili wake kuwasili nchini kesho