Balozi wa Tanzania mjini Tel Aviv nchini Israel Alex Kalua amesema mwili wa marehemu Clemence Mtenga, Mtanzania aliyekuwa akiishi nchini Israel, unatarajiwa kuwasili Tanzania kesho Ijumaa usiku.

Kifo cha kijana huyo kilithibitishwa ijumaa iliyopita na kueleza kuwa kilitokana na shambulizi lililofanywana Oktoba 07 na kundi la Kipalestina la Hamas.

Balozi Kalua, amesema marafiki na jamaa wa Clemence walikusanyika jana na kumuaga marehemu Mtenga.

“Marafiki wa Kitanzania walimuaga marehemu Mtenga, na hivyo tunatarajia mwili wake utafika Tanzania Ijumaa usiku kisha taratibu zingine zitaendelea kutoka hapo.” amesema Balozi Kalua

Kwa Mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya Idara ya mambo ya nje ya Tanzania,Mtenga alikuwa nchini Israel kwa ajili ya programu ya mafunzo ya ndani, na alifariki Oktoba 7.

Hata hivyo mamlaka ilieleza kuwa inafuatilia kwa karibu Mtanzania Joshua Mollel ambaye anadaiwa kushikiliwa mateka. Mamlaka ya Israel awali ilithibitisha kuwa Mollel alikuwa miongoni mwa watu zaidi ya 200 wanaoshikiliwa mateka huko Gaza.

Matokeo darasa la saba yatangazwa ufaulu Hisabati washuka
Mvutano Israel, Hamas wachelewesha usitishwaji vita