Pamoja na shirikisho la soka nchini, TFF kutoa kauli ya kutoitangaza timu iliyopanda daraja kutoka Kundi C katika michuano ya ligi daraja la kwanza, ili kupisha uchunguzi wa upangaji matokeo kufuatia ushindi wa kimbunga kwa timu za Kundi hilo kwenye michezo yao ya mwisho, kocha mkuu wa Geita Gold Sports, Seleman Matola ametuma salamu kwa timu za ligi kuu.

Matola ambaye alikabidhiwa kikosi cha Geita Gold Sports mwishoni mwa mwaka jana, ametuma salamu hizo kwa kuzitaka timu za ligi kuu kutarajia ushindani mkubwa kutoka kwa vijana wake ambao wana uchu wa mafanikio.

Akizungumza akiwa safarini kurejea mkoani Geita, Matola amesema anajisikia furaha sana kutinga Ligi kuu hivyo timu zijiandae.

“Najisikia furaha sana kupanda Ligi kuu” alisema. “Timu zijiandae kwa kuwa ndo kwanza tumepanda” aliongeza Matola ambaye pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Simba SC.

Wakurugenzi wa MSD watumbuliwa Jibu, wadaiwa kufyeka Bilioni
Mbabane Swallows Waichungulia Yanga Ligi Ya Mabingwa