Klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland imeichapa klabu bingwa ya Rwanda, APR kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wenyeji Mbabane Swallows walipata bao pekee na la ushindi kupitia kwa Ndzinisa Sabelo mnamo dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza.

Umahiri wa mlinda mlango wa APR, Olivier Kwizera uliiokoa timu yake kutofungwa mabso zaidi. Kocha wa APR, Emmanuel Rubona atakuwa na kibarua kizito cha kusaka ushindi wa angalau mabao mawili katika mchezo wa marudiano jijini Kigal wiki mbili zijazo.

Mshindi wa jumla wa pambano la APR na Mbabane Swallows atakutana na mshindi wa pambano kati ya Yanga na Cercle d Joachim.

Yanga iliyoshinda Pambano la awali ugenini imejiweka Katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya raundi ya kwanza itakayochezwa mwezi ujao.

Matola Atuma Salamu Ligi Kuu Msimu Wa 2016-17
Stand Utd Waingia Kambini Kuiwinda JKT Ruvu