Maafisa wawili wa Polisi wamepigwa risasi wakati maelfu ya watu wakiandamana katika mji wa Louisville baada ya Mahakama kuamua waliomuua mwanamke mweusi Breonna Taylor wasichukuliwe hatua.
Hasira za waandamanaji zimesababishwa na Bi Taylor mwenye umri wa miaka 26, kupigwa risasi kadhaa baada ya maafisa wa usalama kumvamia nyumbani kwake mwezi Machi.
Maandamano hayo ya yamechochewa na kitendo cha afisa anayeshukiwa kutekeleza mauaji hayo Brett Hankison, kufunguliwa mashtaka tofauti, kinyume na matarajio ya wengi, huku maafisa wengine wawili wakisalia huru bila kufunguliwa mashtaka yoyote.
Kutokana na vurugu zinazoshuhudiwa, hali ya hatari imetangazwa katika mji wa Louisville na jeshi la akiba kutumwa katika mji huo na ripoti zinasema kuwa hali za maafisa hao wawili wa polisi sio mbaya sana na wanaendelea kupokea matibabu, huku mshukiwa akimatwa.
Marekani imeendelea kukumbwa na visa vya mauaji ya watu weusi, vitendo vinavyohusishwa na maafisa polisi wazungu na kuacha maswali mengi kuhusu uwezo wa taifa hilo kupambana na ubaguzi wa rangi.