Chama cha wamiliki wa silaha nchini Marekani (NRA) kimebadili msimamo wake na kuunga mkono udhibiti wa vifaa ambavyo hutumiwa kuimarisha uwezo wa silaha aina ya bunduki ili kuweza kupunguza mauaji nchini humo.
Kifaa hicho cha kuiongezea uwezo bunduki kimekuwa kikitumiwa na wahalifu wengi nchini humo hasa katika kufanya mauaji yanayoendelea likiwemo tukio la mauaji ya watu 50 lililotokea kwenye tamasha Las Vegas.
Aidha, Chama cha Republican kimesema kuwa kitajadili uwezekano wa kupiga marufuku kifaa hicho kinachojulikana kwa jina ‘bump-stock’ ambacho huongeza uwezo wa kufyatua risasi mfululizo.
Kwa upande wake, Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Sarah Sanders amesema kuwa baada ya kutolewa taarifa hiyo ya NRA wanapanga kukutana na vyama hivyo pia na mashirika mbalimbali ili kuweza kufanya mazungumzo ya kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa ni sugu.
-
Watu 50 wauawa kwa risasi kwenye tamasha Marekani
-
Catalonia kujitenga na Hispania
-
FBI yafichua muuaji wa Las Vegas alivyojipanga, wamnasa mpenzi wake
Hata hivyo, Chama hicho kinataka wamiliki wa silaha wenye leseni waruhusiwe kutembea nazo popote pale nchini humo bila kujali utofauti wa sheria katika majimbo wanayotembelea.