Chama cha wamiliki wa silaha nchini Marekani (NRA) kimebadili msimamo wake na kuunga mkono udhibiti wa vifaa ambavyo hutumiwa kuimarisha uwezo wa silaha aina ya  bunduki ili kuweza kupunguza mauaji nchini humo.

Kifaa hicho cha kuiongezea uwezo bunduki kimekuwa kikitumiwa na wahalifu wengi nchini humo hasa katika kufanya mauaji yanayoendelea likiwemo tukio la mauaji ya watu 50 lililotokea kwenye tamasha Las Vegas.

Aidha, Chama cha Republican kimesema kuwa kitajadili uwezekano wa kupiga marufuku kifaa hicho kinachojulikana kwa  jina ‘bump-stock’ ambacho huongeza uwezo wa kufyatua risasi mfululizo.

Kwa upande wake, Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Sarah Sanders amesema kuwa baada ya kutolewa taarifa hiyo ya NRA wanapanga kukutana na vyama hivyo pia na mashirika mbalimbali ili kuweza kufanya mazungumzo ya kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa ni sugu.

Hata hivyo, Chama hicho kinataka wamiliki wa silaha wenye leseni waruhusiwe kutembea nazo popote pale nchini humo bila kujali utofauti wa sheria katika majimbo wanayotembelea.

 

 

Mchungaji aliyemtabiria Mugabe kifo mwezi huu 'ajikwaa'
Diamond 'awafyatukia' wanaodai ana wanawake wengi