Diamond Platinumz ameshindwa kuvumilia makombora ya maneno yanayoelekezwa kwake kuwa anatoka kimapenzi na warembo wengi, hivyo ameamua kujibu kama Simba aliyejeruhiwa.

Kupitia Instagram, Diamond ‘ametoa povu’ akitumia maneno yenye ukakasi akilaani taarifa zinazosambaa juu yake kuwa hajatulia kwani anawabadili warembo na kuumiza mioyo yao.

Baba Tiffah amesema kuwa hajatoka kimapenzi na mwanamke yeyote na hana  uhusiano wa kimapenzi na mrembo yeyote zaidi ya Zari ambaye hivi sasa yuko nchini Afrika Kusini.

Mondi alitamba kuwa hakuna kinachomzuia kuwa na wanawake wengi kwani bado ana umri mdogo na kwamba imani yake ya dini inaruhusu kuwa na wanawake hadi wanne, hivyo ukifika muda utaratibu utafuatwa.

“Sina Mahusiano na Yoyote anaetajwa, na Siku pia Nikimaliza Mahusiano yangu na Alie South na nikawa na Mwengine na ikifikia kuliweka wazi ntaliweka wazi Mwenyewe, Maana hakuna kitachonizuia… ndio kwanza nna miaka 28, Sijaoa na Hata nikioa Naruhusiwa niwe na wake Wanne PERIOD!!!….” Yanasomeka baadhi ya maandishi ya Mondi.

Haya yameibuka wakati kukiwa na tetesi kuwa mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu ameonekana akiwa nyumbani kwake Madale, huku Hamisa Mobeto akidaiwa kufungua kesi dhidi yake akidai matunzo ya mwanae.

Diamond alijibu kwa mapana kama ‘mtupa jiwe gizani’ bila kugusa kitufe kimoja kinachozungumziwa.

Mauaji yazidi kuwapasua vichwa wamiliki wa silaha
George Weah atiliwa shaka Liberia baada ya kuwasiliana na Taylor