Nyota wa zamani wa soka Geoge Weah ambaye ni mmoja wa wagombea wa urais nchini Liberia, amekiri kuwa na mawasiliano na kiongozi wa zamani wa taifa hilo Charles Taylor.

Charles Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makossa uhalifu wa kivita baada ya kuhukumiwa na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa na kuna hofu ya Taylor kuwa na ushawishi katika uchaguzi.

George Weah mesema kuwa ni kweli alipokea simu kutoka kwa Taylor lakini akakanusha madai ya Taylor kuwa na ushawishi wa mambo nchini humo.

Bunge la Congress nchini Marekani liliidhinisha azimio la kushutumu juhudi zozote za mbabe huyo wa zamani wa kivita za kujaribu kuwa na ushawishi kwenye uchaguzi nchini Liberia.

George Weah ni mmoja wa wagombea 11 ambao wamejitokeza kutaka kumrithi Rais Ellen Johnson-Sirleaf ambaye anastaafu wakati mke wa zamani wa Charles Taylor, Jewel Howard-Taylor ni mgombea mwenza wa George Weah.

Makamu wa rais wa Johnson Sirleaf, Joseph Boakai, pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumanne tarehe 10 Oktoba.

Kuna mwanamke mmoja pekee aliyejitokeza kuwania, MacDella Cooper, ambaye alikuwa mwanamitindo lakini kwa sasa ni mfanyakazi wa hisani.

 

Diamond 'awafyatukia' wanaodai ana wanawake wengi
CIA waichambua akili ya kiongozi wa Korea Kaskazini