Mawakili wa Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya IEBC na wale wa Rais Uhuru Kenyatta kesho wanatarajiwa kuwasilisha stakabadhi katika mahakama ya upeo, ili kujibu mashtaka ya John Harun Mwau, Njonjo Mue na Khelef Khalifa wanaotaka matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita yafutwe na zoezi hilo lianze kuandaliwa upya.
Mawakili hao wamekuwa katika pilika pilika za kuwianisha hoja zao, huku Dkt. Ekuru aukot, aliyewania nafasi ya urais mwezi uliopita na kubwagwa, hivyo amewasilisha ombi la kujumuishwa kwenye kesi hizo mbili.
Aidha, katika uchaguzi wa marudio uliopita na kususiwa na kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani (NASA}, Raila Odinga, ulimpatia ushindi mkubwa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.
Hata hivyo, kwa upande wake Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo limepiga hatua kubwa katika suala zima la Demokrasia kwani imeonyesha mfano bora na kuigwa hivyo amewataka vyama vya upinzani kuheshimu maamuzi ya wananchi.