Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Young Africans Fiston Kalala Mayele, ameliteua Bao la ushindi dhidi ya Azam FC kuwa bao Bora miongoni mwa Mabao aliyofunga msimu huu, katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mayele ametoa kauli hiyo, baada ya kuiwezesha Young Africans kurejesha heshima ya Ubingwa jana Jumatano (Juni 15), kwa kuifunga Coastal Union 3-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza na Azam TV baada ya mchezo huo, Mshambuliaji huyo alisema licha ya kufikisha mabao 16 katika Ligi Kuu, bado anaamini bao aliloifunga Azam FC katika mchezo wa mzunguuko wa pili uliopigwa kwenye Uwanja wao wa Azam Complex, ni bao bora kwake.

“Bao nililowafunga Azam FC pale Chamazi kwangu ni bao bora zaidi, nimefunga mabao mengi msimu huu, lakini lile lilikua zuri zaidi.” Alisema Mayele

Katika mchezo wa jana Jumatano (Juni 15) Mayele aliifungia Young Africans mabao mawili, huku bao lingine likifungwa na Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Chiko Ushindi.

Hadi sasa Mayele anaongoza orodha ya wafungaji katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, akifuatiwa na George Mpole mwenye mabao 14.

Diamond ampongeza Manara, Young Africans
Simba SC imeanza na Moses Phiri, yamtambulisha rasmi