Klabu ya Mbeya City imefikia makubaliano na Kocha Nsanzurwimo Ramadhani kuwa Kocha Mkuu kwa mkataba wa awali wa Msimu mmoja wa ligi kuu ya Vodacom inayoendelea.

Kocha Ramadhan ni raia wa Burundi na anatarajia kujiunga na timu huko kanda ya ziwa inakoendelea na michezo ya ligi kuu.

“Ramadhan ni coach mzuri. Anapenda sana tiki taka. Aliwahi kuwa coach wa Kiyovu Sport team ya hapa Rwanda. He likes entertaining football. All the best to Rama.”  Maneno ya mchezaji mahiri wa zamani na Mwandishi wa habari Mwandamizi nchini Rwanda, Gakuba Abdul Djabar ‘Romaria’.

Kocha Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika vilabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini, pia amewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi na kocha msaidizi/kocha mkuu wa Muda (care-taker) kwa timu ya taifa ya Malawi.

Azam FC kuifuata Singida Utd kesho
Mwakyembe: Nataka mkandarasi mpya wa kutoa tiketi uwanja wa taifa utakapofunguliwa