Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu wa Chadema, Edward Lowassa leo January 8, 2018 wamefika hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa wake.

Mzee Kingunge amesema anaendelea vizuri na anatarajia kutoka jumatano na kushiriki mazishi ya mkewe.

“Wakati madaktari wananisafisha haya majeraha nikawauliza, kama mimi nasikia maumivu hivi, Lissu je ana maumivu kiasi gani?,  amesema mzee Kingunge

Hata hivyo madaktari wamesema hali ya mwanasiasa huyo mkongwe inazidi kuimarika licha ya maumivu anayopata kutokana na majeraha aliyonayo.

Simba SC yatupiwa virago Mapinduzi Cup
Ummy Mwalimu awapa hamasa Coastal Union