Mahakama ya Malindi ilimuachilia huru Mhubiri tata Paul Mackenzie na washtakiwa wengine tisa waliokuwa wameshitakiwa pamoja naye.

Jaji wa Mahakama hiyo, Ivy Wasike alisema kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo wala kuwapa dhamana washukiwa hao hivyo kufunga mashtaka yaliyokuwa yakiwakilibili washtakiwa hao.

Hata hivyo Mackenzie na wenzake walikamatwa tena muda mchache baada ya kuachiliwa huru na wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Shanzu.

Mchungaji Paul Mackenzie alifikishwa Mahakamani Aprili 17, 2023 akituhumiwa kuwashawishi waumini wake kufunga kula na kunywa hadi wafe, ili wakakutane na MUNGU wao akidai mwisho wa dunia utakuwa Juni mwaka huu.

ASFC-Simba SC yaitangazia vita Azam FC
Tajiri PSG amuwekea masharti Sergio Ramos