Raia wa Marekani DK. William Morris amemshitaki mchungaji Josephat Mwingira kwa kuzaa na mke wake Dk. Nyimbi, hivyo ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuamuru mchungaji huyo kwenda kupima vina saba DNA.

William Morris amelazimika kufanya hivyo ili kujua baba mzazi wakiumbe kilicho zaliwa na mke wake DK. Nyimbi miaka tisa iliyopita.

Maombi hayo yamewasilishwa jana kupitia wakili wake Respicius Ishengoma.

Baada ya mahakama kupokea maombi hayo, imetoa siku 14 kwa mchungaji Josephat Mwingira kujibu kisha usikiliozwaji uanze na kutolewa uamuzi .

Aidha Dk. Morris amewashitaki Mchungaji Mwingira na Dk. Nyimbi na kudai kuwa endapo watakutwa na hatia alipwe fidia ya sh bilioni 7.5 kwa mchungaji huyo kuzini na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkewe.

Video: mimi nilishakuwa maarufu kabla ya Yanga-Jerry
Video: Mwakyembe ameumia sana - Talimba