Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (SportPesa), Abbas Talimba amesema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe amepata pigo kubwa sana na yupo katika kipindi kizito kwani ameumia sana.

Talimba amesema kufiwa si jambo jepesi na nisafari ambayo aliyeenda hawezi kurudi, hivyo ni kitu kikubwa sana na hili limekuwa pengo kubwa sana kwa Dkt. Mwakyembe.

Mwili wa marehemu Linah Mwakyembe umeagwa jana jijini Dar es salaam na kusafirishwa kwenda Kyela mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi, wakati wa kuaga mwili huo, Waziri Mwakyembe alishindwa kujizuia na kujikuta akilia juu ya jeneza la mke wake marehemu Linah Mwakyembe.

Mchungaji Mwingira ashitakiwa kuzaa na mke wa mtu
Torino Football Club Wamshukuru Joe Hart