Rais wa klabu ya Torino ya Italia Urbano Cairo, ametoa shukurani kwa mlinda mlango Charles Joseph John (Joe Hart), ambaye alitumikia klabu hiyo kwa mkopo msimu wa 2016/17, akitokea Man City ya nchini kwao England.

Cairo amesema hawakutarajia makosa kutoka kwa Hart ambaye alilazimika kuondoka Man City, kufuatia meneja wake Pep Guardioa kuzungumza mapungufu ambayo aliyaona kwa mlinda mlango huyo, siku chache baada ya kuanza maandalizi ya msimu uliopita.

Kiongozi huyo wa Torino amesema waliishi vizuri na Hart, na hawakuwahi kupata ripoti mbaya kutoka kwa viongozi wa benchi la ufundi ambalo siku zote limekua karibu na wachezaji wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Italia (Sirie A).

“Hart alifanya makosa ya kwaida, tofauti na alivyokua akizungumzwa wakati tunamsajili kwa mkopo akitokea Man City,” Amesema Cairo

“Alikua na umuhimu mkubwa sana kwetu kwa kipindi chote cha msimu uliopita. Na hakuna yoyote kati yetu ambaye alitarajia kuona akifanya makosa katika kazi yake.”

Urbano Cairo ametoa pongezi hizo kwa Joe Hart, siku moja baada ya mlinda mlango huyo kukamilisha mpango wa kujiunga na wagonga nyundo wa jijini London (West Ham Utd) kwa mkopo akitokea Man City.

Video: Mwakyembe ameumia sana - Talimba
Video: Tumepata pigo kwa kuondokewa na mke wa Dkt. Mwakyembe-DC Hapi