Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa wamepata pigo kubwa kuondokewa na mke wa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Linah George Mwakyembe kilichotokea jijini Dar es salaam.

Ameyasema hayo wakati wa Ibaada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika jijini Dar es salaam, ambapo amsema kuwa ni vigumu kuzoea hali hiyo, lakini ikishatokea ni kukubaliana na uhalisia tu.

“Dkt. Mwakyembe amepata pigo kubwa sana kama mume, lakini si kwake tu bali kwa ndugu, jamaa na marafiki kwani hali ya msiba siku zote huwa haizoeleki, lakini ikishatokea hatuna budi kukubali uhalisia, hivyo msiba huu umemgusa kila mtu,”amesema Hapi

Aidha, amesema kuwa miaka kadhaa iliyopita Linah Mwakyembe alifanya kila njia kupigania afya ya Dkt. Mwakyembe alipokuwa anaumwa, lakini leo hali imebadilika na kugeukia upande wa pili.

Hata hivyo, Hapi ameongeza kuwa wao kama vijana wamepoteza mama shupavu na aliyekuwa mlezi mzuri wa maadili, hivyo kilichobaki ni kumuombea Waziri Dkt. Mwakyembe asiweze kutetereka kwa hicho kilichotokea.

 

Torino Football Club Wamshukuru Joe Hart
Kisa cha mke kufyeka sehemu za siri za mumewe