Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina Lionel Messi, amepanga kurudi kwenye timu yake ya utotoni ya Newell’s Old Boys, mara baada ya mkataba wake na Inter Miami kumalizika.

Messi ambaye mkataba wake huo Unata rajiwa kumalizika mwaka 2025, anawindwa pia na baadhi ya timu kutoka Saudi Arabia ambazo zimepanga kumsajili baada ya mkataba wake na Miami kumalizika.

Matajiri hao wa Saudia waliweka mezani ofa miaka mitatu ambayo kwa mwaka ingemfanya Messi kupata Euro 500 milioni, hivyo kwa miaka mitatu angejipatia Euro 1.5 bilioni kwenye mshahara tu.

Awali staa huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 36, alihusishwa huenda angerudi kwenye kikosi cha Newell’s kabla hata ya kutimkia Marekani.

Messi ametua Miami katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu, amekuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa timu hiyo akiwa amefunga mabao 11 kwenye mechi 12 za michuano yote alizocheza hadi sasa.

Ziara ya Rais India: Tanzania kuanzisha Kiwanda cha Simu janja
Robertinho anataka mambo mawili Mbeya