Katika kuhakikisha kunakuwepo na mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu mashuleni, Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameahidi kuchangia mifuko 100 ya Simenti pamoja na Mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Maweni iliyopo Kata ya Mjimwema wilayani Kigamboni.

Mwita amesema kuwa hatua hiyo ni kwa ajili ya kuzisaidia shule ambazo zina upugufu wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi wasome katika mazingira salama.

“ Kama kwenye Kata yako unaona kabisa wanafunzi wanakaa chini na wewe diwani upo, basi ujue huna sifa ya kuwa diwani na wananchi watakuwa na haki ya kukuondoa madarakani kwenye uchaguzi ujao,”amesema Mwita.

Aidha, amesema kuwa jambo la uchangiaji wa kusaidia wanafunzi wasikae chini sio la kisiasa bali ni katika sehemu ya kuwasaidia wananchi hivyo kuwataka wananchi kuondoa dhana ya kisiasa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema, Selestine Maufi amempongeza Meya Isaya kwa kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule hiyo.

Hata hivyo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Selemani amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba kadhaa vya madarasa ambapo vilivyopo havikidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo.

 

Video: Siri ya ushindi wa Lissu TLS, Kingunge awataja vigogo watatu wasaliti CCM
Video: Diamond Platnum aukwaa ubalozi wa GSM Mall