Ng’ombe huyu alikuwa na sentimita 190 (inchi 74.8), akiwa ndiye Ng’ombe mrefu zaidi kuwahi kutokea duniani na kuingizwa katika Guinness World Records.
Ng’ombe huyu aliishi kwenye shamba moja huko Orangeville, Illinois nchini Marekani. Mmiliki wake, Patty Meads-Hanson, alimpatia jina la Blosom wakati Ng’ombe huyo alipokuwa na umri wa wiki nane huku jambo la kushangaza likiwa ni jinsi ambavyo alikuwa hajali watu walivyokuwa wkijaa na kushangaa.
Alipofikisha umri wa miaka 13 alifariki, hiyo ilikuwa Mei 26 kutokana na jeraha alilolipata kwenye mguu wake wa kushoto, wakati akichunga kwenye malisho.
Madaktari wawili wa mifugo walifanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanaokoa uhai wa Ng’ombe huyu lakini hawakufaulu baada ya kuumia alipoteleza kwenye tope na kushindwa kusimama kutokana na mishipa ya nyonga kupata hitilafu.