Kikosi cha KMC FC kimeelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 15, mwaka huu.

Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema timu hiyo ilianza zoezi la kupima afya tangu jana Jumapili (Julai 16), ambapo ratiba inayofuata ni kuelekea Zanzibar ambako wataweka kambi ya majuma mawili.

“Tayari tumeshaiona kalenda ya matukio ya msimu ujao na baada ya kuona mwongozo huo timu ilianza taratibu za kupima afya wachezaji na baada ya hapo leo Jumatatu kikosi kimeondoka kwenda Zanzibar kuanza kambi ya majuma mbili.

“Tukitoka huko, tutarejea Dar es Salaam kabla ya kwenda Morogoro nako kutulia kidogo katika kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa 2023-24 tukihitaji kufanya vizuri na baada ya kurudi Moro sasa tutakuwa tunasubiri ratiba kamili ya ligi kwamba tunaanza na nani,” amesema Mwagala.

Mikoa vinara ulimaji wa Bangi, Mirungi yawekwa hadharani
Mfahamu Ng'ombe mrefu zaidi Duniani