Kocha wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Thomas Tuchel ameweka wazi nafasi ya Mshambuliaji kutoka Senegal Sadio Mane ni ndogo sana kwenye kikosi chake kwa msimu ujao 2023/24.

Mabingwa hao wanajiandaa kumpiga bei Mane kwa kitita cha Pauni 17 milioni kipindi hiki cha usajili wa kiangazi, ili wapate pesa ya kuongezea kwa ajili ya kunasa saini ya Harry kane.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari, Tuchel alisema Mane anapitia kipindi kigumu Bayern baada ya kujiunga kwa Pauni 35 milioni akitokea Liverpool.

Kwa mujibu wa Sportl, Tuchel alisema: “Hakuwa na matarajio makubwa baada ya kujiunga, ushindani ni mkali sana, nafasi ya kikosi cha kwanza imekuwa ngumu na mchezaji anaelewa pia, anaelewa mawazo yangu na klabu kwa ujumla.’

Mane alivumilia kipindi chote kigumu alichopitia akiwa na Bayern, tangu alipotua baada ya kudumu kwa muda wa wiki sita.

Mane aliondoka Liverpool baada ya kudumu miaka sita na kupata mafanikio makubwa.

Bayern imepania kunasa saini ya Kane kwa kitita cha Pauni 70 milioni, lakini inaonekana kama Tottenham haipo tayari kumuuza kipindi hiki cha usajili wa kiangazi.

Kwa mujibu wa ripoti Tottenham inajiandaa kuigomea ofa nyingine ya Bayern ambayo imepanga kutuma, imeelezwa klabu hiyo inaamini Kane ana thamani ya Pauni 120 milioni.

Kwa sasa Bayern inajiandaa kuuza baadhi ya wachezaji wake kama Marcel Sabitzer kwa Pauni 12 milioni, na Benjamini Pavard ambaye huenda akauzwa kwa Pauni 34 milioni. Mchezaji ghali ambaye yupo katika orodha ya watakaopigwa bei dirisha hili la kiangazi ni Ryan Grayenberch, ambaye anapatikana kwa Pauni 42 milioni.

Wakati huo huo Bouna Sarr, Alexander Nubel na Yann Sommer wanatarajia kuondoka na uhamisho wao hauzidi Pauni 8.5 milioni.

Mfahamu Ng'ombe mrefu zaidi Duniani
Peter Banda Out, Miquissone In