Mfalme Charles III ameahidi kulitumikia taifa hilo kwa uwajibikaji kama mama yake katika kipindi cha utawala wake wa miaka 70.

Katika hafla ya kumtangaza zilizoanza leo Jumamosi Septemba 10, 2022 katika kasri la St. James’s jijini London ameahidi kumfuata kipenzi mama yake kujitolea maisha kuhudumia jamii na dunia.

Baraza la Viongozi lenye jukumu la kumtangaza mfalme linaloundwa na wanasiasa wa ngazi ya juu na maafisa ambao wanamshauri mfalme lilifanya kazi hiyo na imeoneshwa moja kwa moja katika televisheni ikiwa ni kwa mara ya kwanza.

Mfalme Charles III akisaini kiapo mbele ya mkewe, Camilla na mwananawe Mwanamfalme William

Baraza hilo lilikutana kabla, bila ya Charles kuwepo wakati linatangaza rasmi jina la mfalme mpya kama mkuu wa nchi kuwa ni Mfalme Charles III.

Charles, mwenye umri wa miaka 73, mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth II na ambaye ni baba wa William na Harry, alichukua kiti cha ufalme moja kwa moja mara tu baada ya kifo cha mama yake Malkia Elizabeth II, kilichotokea Septemba 8, na hafla ya kutangazwa rasmi Jumamosi ni hatua muhimu ya kikatiba na uthibitisho wa utambulisho wake kama mfalme mpya wa Uingereza.

Wakati hafla hiyo ikianza Mfalme mwenyewe hakuweko, lakini alihudhuria awamu ya pili ya shughuli hiyo ya kikao chake cha kwanza cha baraza kuu.

Kiongozi wa chama cha Labour, Keir Starmer akiwa na mawaziri wakuu wastaafu, Tony Blair, Gordon Brown na Boris Johnson

Karani wa baraza hilo Richard Tilbrook alitangaza, “Charles Mfalme, kiongozi wa jumuiya ya madola, mlinzi wa imani”, kabla ya kutangaza “God Save the King” yaani Mungu mlinde mfalme. Chumba kilichojaa watu akiwemo Malkia – mkewe mfalme, mwanamfalme wa Wales na Waziri mkuu Liz Truss, waliirejelea kauli hiyo.

kitoa tangazo lake mwenyewe, Mfalme alisema, “Waheshimiwa, wake kwa waume, ni kwa wajibu na huzuni nawatangazia kifo cha mamangu mpendwa, Malkia,”

Aliendelea, “Nafahamu jinsi nyinyi, taifa zima na nadhani naweza kusema dunia nzima imehuzunika pamoja nami kwa kuondokewa huku. Ninafarijika pakubwa kwa risala za wengi kuelezea huzuni kwa dadangu na kaka zangu.

Mfalme amekiri kuwa Maisha yake yamebadilika sasa, akieleza kuwa hatoweza kutoa “muda zaidi na nguvu” kwa wakfu mbali mbali na masuala ambayo alitoa usaidizi kwa miongo kadhaa kama mrithi wa kiti cha enzi.

Simba SC yakiwasha ugenini
Wafugaji washauriwa kununua ardhi, kufuga kisasa