Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ni msikivu na anajali wananchi wa hali zote bila ubaguzi wowote.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kigamboni waliokuwa wamejitokeza kufyeka pori la NAFCO lililoko kata ya Somangila, eneo ambalo ni hatarishi kwa usalama wa raia.
Aidha, Mgandilwa amewashukuru wananchi kwa kuwa watulivu kwa muda wote ambao walikuwa wakilalamikia pori hilo huku serikali ikiwataka wawe na subira wakati taratibu za ufutaji zinaendelea.
“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni sikuvu inayodhamiria kuleta maendeleo kwa wananchi, ndiyo maana Rais Magufuli amesikia kilio chenu na kuamua kuifuta hati ya Shamba hili ili liwe mikononi mwa serikali, tuendelee kuiunga mkono serikali na sitaki kuona mtu anafanya siasa katika hili, tufanye kazi,”amesema Mgandilwa
Vile vile, Mgandilwa amwapa wananchi wiki moja kuanzia leo kuendelea kusafisha eneo hilo kwa kufyeka vichaka na kukata miti kwa matumizi yao ya nyumbani kama kuni au shughuli za ujenzi.
-
Dkt. Mwakyembe apiga marufuku matumizi ya takwimu GeoPoll
-
Gazeti la Raia Mwema lafungiwa kwa siku 90
-
Muhimbili yapongezwa kwa kutoa huduma bora
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndungulile amewataka wananchi kuendelea kushikamana kwa Umoja katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwani Kigamboni itajengwa na wote. Pia amewaomba wananchi waendelee kuiunga mkono serikali yao kwani imetatua kero zao kubwa pamoja na Rais Magufuli kuifuta mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) ambayo ameipigia kelele kwa muda mrefu bungeni