Mgonjwa wa kwanza mwenye maambukizi ya Virusi vya Corona amegundulika nchini New Zealand taarifa iliyotolewa leo februari 28 na Waziri mkuu wa nchi hiyo Jacinda Ardern imethibitisha kuwa nchi yake imekuwa na mgonjwa mmoja mwenye maambukizi ya virusi hivyo.

Mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 60 amegundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo baada ya kupata vipimo na anatibiwa katika hospitali mjini Auckland, ambapo amesema kuwa mgonjwa huyo alirejea nchini humo hivi karibuni kutoka nchini Iran

Nchi nyingine ambazo zimeripotiwa kuwa na maambukizi ya corona hivi karibuni ni Italia, Iran na korea kusini.

Ikumbukwe kuwa ugonjwa huo ambao umekuwa ni tishio ulianza nchini China disemba 2019 na kwa hivi sasa ugonjwa huo umeenea zaidi ya nchi 40

 

Raia wa Afrika kusini waliopo China kurejea makwao
Henga: watumishi wa LHRC wanapewa vitisho