Kiungo wa klabu ya Man Utd, Michael Carrick amekanusha madai kuwa wachezaji wa klabu hiyo hawachezi vizuri ili kuharibu kibarua cha kocha wao.

Wachezaji wa Man United walilalamikiwa baada ya kupoteza mchezo wa nne mfululizo dhidi ya Stoke City kwa kuchapwa mabao 2-0 Jumamosi ya majuma mawili yaliyopita.

Carrick amesema ni makosa kusema wachezaji hawajitumi kadri ya uwezo, inaumiza sana na akasema kwamba wao sio watu wa aina hiyo.

“Tunapambana kwaajili ya timu na  kwa ajili ya kocha wetu Louis Van Gaal, hakuna mpango wa kumwangusha,” alisema Carrick.

“Inaumiza sana kuambiwa kwamba hatujitumi ili kulinda kibarua cha kocha wetu, sisi so watu wa aina hiyo,” aliongeza nahodha huyo msaidizi.

 

Obama amwaga machozi akitoa hotuba Ya umiliki wa Silaha za Moto
Uwanja Wa Amani Zanzibar Waandika Histoaria Mpya