Afara Suleiman, Hanang’ – Manyara.
Miili 47 ya wakazi wa mji wa Katesh na Kijiji cha Gendabi waliokufa baada ya Mvua kunyesha kwenye kilele cha Mlima Hanang’ Mkoani Manyara, inatarajiwa kuangwa hii leo Desemba 4, 2023 majira ya saa kumi za alasiri kwenye viwanja vya michezo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia ndiye anatajwa kutarajiwa kuongoza uagaji wa miili hiyo sambamba na Viongozi wengine waliopo eneo hilo akiwemo Waziri wa Maji, Innocent Bashungwa, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi na utawala Bora, Jenista Mhagama.
Vyombo vya ulinzi na usalama vikiongozwa na Jeshi la Wananchi JWTZ, vinaendelea na shughuli za uokoaji na mapema hii leo majira ya asubuhi Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel aliwatembelea waathiriwa wa tukio hilo Hospitalini na kusema tayari Madaktari wapo eneo la tukio kwa ajili ya usaidizi wa kitabibu.
Hadi kufikia sasa, majeruhiwa 85 wanaendelea na matibabu na wanannchi wameombwa kuwa watulivu wakati utaratibu wa uokozi ukiendelea huku wakitakiwa kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki ambapo mvua bado zinaendelea kunyesha.