Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali imeweka kipaumbele katika kuimarisha huduma za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema kupitia mifumo, Sera na Teknolojia.

Amesema hayo wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Mawaziri la Majadiliano ya Juu la Utekelezaji wa Tahadhari ya Mapema kwa Wote katika Mpango Kazi wa Afrika lililofanyika pembeni ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Dkt. Jafo amesema Serikali inahakisha inapunguza athari za majanga kwa kuboresha ustawi na uthabiti wa watu wake na jamii kama sehemu ya mkakati wa maendeleo kwani majanga matokeo ya maafa yanaathiri mipango na malengo ya maendeleo yake.

“Ni muhimu kujiandaa kupitia mifumo ya tahadhari ya mapema inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa athari na kuokoa maisha ya watu na mali nyingi na kwa umuhimu huo Tanzania imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026) pamoja na Mchango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NDC),” amesema.

Hata hivyo, Dkt. Jafo amesema imeanzishwa shahada katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu masuala ya Hali ya Hewa na Mabadiliko ya Tabianchi, kusaidia kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu nchini hasa kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Miguel Gamondi: Tulijiamini kupita kiasi
Miili 47 waliokufa kwa mafuriko kuagwa leo