Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 17, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Daraja la mawe katika barabara ya Iguguno-Kikhonda-Kinampundu, lenye urefu wa mita 30, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida

Daraja hilo limejengwa kwa kutumia teknolojia rahisi ya mawe kwa gharama ya shilingi milioni 102.

Ujenzi wa daraja hili ni sehemu ya kazi zilizofanyika katika Mkataba wa Matengenezo ya muda maalumu ya barabara ya Mwando – Miganga – Kinandili yenye urefu wa kilomita 12.39, kazi zote zimegharimu kiasi cha fedha shilingi milioni 444.

Aidha Waziri Mkuu amewapongeza wakandarasi kwa ubunifu wa daraja hilo na kuagiza wapewe kazi ya ujenzi wa madaraja mengine.

Meneja wa TARURA mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David amesema ujenzi wa daraja hilo utasaidia kuondoa changamoto ya mawasiliano iliyokuwepo kwa wananchi hasa kipindi cha masika.

Majaliwa 'amkubali' mkandarasi Daraja la mawe
Mapigano ya kikabila yasababisha vifo 33