Katibu mkuu wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas ametangaza neema kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu nchini kupitia makusanyo ya fedha za wasanii (Mirabaha) kutoka katika maeneo mbali mbali ambayo kazi za sanaa zinatumika. 

Dkt Abbas ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalumu na Dar24 Media alipohudhuria mashindano ya Miss and Mr Deaf Africa 2021 yaliyofanyika tarehe 1 oktoba 2021 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dare es salam.

Abbas amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa mfumo bora wa kukusanya Mirabaha na hadi kufikia mwezi Desemba mwaka 2021, Wizara kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) itaanza utaratibu rasmi wa kuwapatia wasanii stahiki zao


”Tunakuja na kanuni zitakazokusanya zaidi fedha za wasanii kwenye vyombo vya habari kama Redio na Tv na hilo wadau wote wametoa maoni, hoja ikawa kiwango gani, ila tumeshakubaliana na wadau tunaanza na tozo ndogo hivyo tukutane Desemba watu wachue cheki zao” alisema Abbas.

Aidha Dkt Hassan Abbas ametoa rai kwa wasanii wote nchini kuhakikisha wanajisajili chini ya chama cha Haki miliki Tanzania ili kuwa na sifa za kuingia kwenye mfumo.

”Wasanii wao waendelee kutengeneza kazi bora, kwa sababu dhana ya Copy rights ni kwamba usajili kazi yako, na wahakikishe kazi zao zinasikika na kuangaliwa katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni” Alisema Abbas

Wasanii mbalimbali nchini wamekua wakilalamika kutopata maslahi yanayoendana na kazi wanazozifanya na kuona wanaibiwa kazi zao bila mafanikio

Billioni 50 kujenga bandari ya kilwa
R Kelly afungiwa YouTube