Video iliyosambazwa kweye mitandao ya kijamii hivi karibuni ikimuonesha askari wa jeshi la polisi akiomba rushwa kwa raia wa kigeni (mtalii) imemfukuzisha kazi askari huyo.

Jeshi la polisi visiwani Zanzibar, jana lilimsaka na kumkamata askari  huyo aliyetambulika kwa jina la Sajini Hamadi Kassim wa kituo cha Mkokotoni visiwani humo na baadae kumfuta kazi akisubiri hatua nyingine za kisheria.

Kupitia kipande cha video hiyo iliyosambaa, alionekana akiomba na kupokea rushwa ili aweze kumsamehe raia huyo wa kigeni kwa kosa la kutofunga mkanda.

Askari huyo ambaye alionekana kutoelewana na raia huyo wa kigeni aliyeapa kutorudi tena Zanzibar kutokana na kuharibiwa siku yake ya mapumziko, alifanya mazungumzo muda wote na mwanamke aliyekuwa kwenye gari hilo.

“I will never come back to Zanzibar… ever (Sitarudi tena Zanzibar… milele),” alisema raia huyo wa kigeni huku akipoozwa na askari huyo aliyekuwa akiwaelekeza namna ya kuwakwepa askari wenzake huku muda wote mkono wake ukielekea kwenye pesa aliyoiomba.

Askari huyo alioekana akipokea fedha za kitanzania zinazoaminika kuwa ni rushwa ya shilingi 60,000.

ATCL yagusia Ratiba ya safari za ndege mpya, abiria walia na pengo la Fastjet
Profesa Lipumba apata pigo lingine CUF