Mvutano wa kiti cha uenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) umeendelea kuchukua sura nyingine baada ya Profesa Ibrahim Lipumba anayedai kuwa ndiye mwenyekiti halali aliyetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini kupata pigo lingine la kukataliwa.

Siku moja baada ya msomi huyo kutangaza uteuzi wa bodi nyingine ya udhamimini ya chama hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya chama hicho, Abdallah Khatau ametangaza kutomtambua.

Akiongea na waandishi wa habari jana katika ofisi za makao makuu ya CUF visiwani Zanzibar, Khatau alisema kuwa kwa kutambua wajibu wao kikatiba, hawamtambui Profesa Lipumba kutokana na kutambua uamuzi wa kikatiba wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho kumvua uanachama.

“Profesa Lipumba sio mwenyekiti wa CUF na wala sio mwanachama kwa sababu tayari ameshavuliwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa,” alisema Khatau.

Juzi, Profesa Lipumba alitangaza kumteua Thomas Malima na kumtaka kuitisha kikao cha Bodi ya Wadhamini. Sambamba na hilo, alitangaza kuwatimua baadhi ya wakurugenzi wa idara za chama hicho.

Mitandao yamtumbulisha Polisi aliyeomba rushwa kwa mtalii Zanzibar
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo awasili nchini kwa ziara ya siku tatu