Serikali nchini, imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara zinazotumika kupeleka watalii katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, kwa kushirikiana na wadau na mamlaka zinazohusika kwa lengo la kuwawezesha watalii wanaotembelea hifadhi hiyo kufika kwa urahisi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuboresha barabara zote zinazowapeleka watalii mlima Kilimanjaro.

Amesema, miongoni mwa jitihada zilizofanyika za kuboresha miundombinu ya barabara katika hifadhi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara za Machame, Mwika na Marangu kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri Masanja ameongeza kuwa, “Serikali naendelea kufanya ukarabati wa mara kwa mara wa barabara za changarawe zinazoelekea katika lango la Rongai, Lemosho, Kilema, Londorosi na Umbwe.”

Mahakama yamuachilia huru Lengai Ole Sabaya
Aliyepona Marburg alia kuwapoteza ndugu, mama mzazi