Mlipuko mkubwa umetokea katika kituo cha mafuta nchini Ghana katika mji mkuu wa Accra ambapo imeripotiwa kuwa watu watatu wamepoteza maisha.
Taarifa zinasema kuwa mlipuko huo ulirusha moto mkubwa angani na kuwalazimu watu waliokuwa karibu na eneo hilo kukimbilia eneo la makutano ya Atomic, kaskazini mashariki mwa mji huo.
Mlipuko huo uliripotiwa kusababishwa na Lori lililokuwa limepeleka gesi eneo hilo kushika moto na kusababisha mlipuko wa kituo cha petroli.
-
Kichwa cha mwandishi wa habari chapatikana baharini
-
Jeshi la Polisi lawatupia lawama panya kwa upotevu wa mihadarati
-
Video: Makamba, Nchemba, Mwakyembe, wapeta baraza jipya la mawaziri
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani nchini Ghana Kojo Oppong Nkrumah baad ya moto kuanza kusambaa kwenye mtaa wa Legon ulidhibitiwa kwa haraka na watu watatu walithibitiswa kufariki na takriban wengine 30 walijeruhiwa.
Mwaka 2015 karibu watu 150 waliuawa kwenye moto wa kituo cha Petroli mjini Accra.