KUNRADHI

Ni desturi ya waungwana kuomba radhi pale anapokosea ama jamii yake inapokosea dhidi ya jamii nyingine,

Huu ndio uungwana hususan kwa malezi bora tuliyoyapata toka kwa wazazi na walezi wetu,

Narudia kusema kunradhi kwa wote walioguswa na kauli zisizo za kistaarabu zilizotolewa na msemaji wa klabu ya Yanga bwana Jerry Muro dhidi ya wakazi na wenyeji wa Dar es salaam, Muro alifika mbali zaidi kwa kutoa kejeli dhidi ya wazaramu, siwezi kuyarudia humu kwani nitakuwa nazidi kukejeli,

Nachukua nafasi hii kuwaomba radhi wale wote waliokwazwa na kauli hizo ambapo nami ni mmoja wao, maana nami ni mzaramu isitoshe ni mzaliwa wa hapa Dsm,

Ndugu zangu binafsi na kwa niaba ya walio wengi tunaomba mtusamehe sana, maana ni dhahiri inaonekana ni kauli ya klabu ya Yanga, kutokana na kusemwa na msemaji wetu wa klabu yetu, ukiangalia video utaona msemaji alizungumza kwenye sehemu maalum ya kauli za Yanga,

Najua kuwa Yanga ina utaratibu wake katika kufuatilia na kushughulikia yale yahusuyo nidhamu, hata pia utaratibu wa usemaji,

Kunradhi hii aina uhusiano wa kimamlaka juu ya yanga, huu ni utashi wa kiungwana kama nilivyosema awali, pia hakuna uhusiano wowote na kauli zinazohusu wanamichezo ama timu zilizotajwa kwenye kadhia hiyo, kilichoguswa humu ni maneno ya kejeli, dharau na udhalilishaji kwa wazawa na zaidi wazaramu, nikichukulia kuwa hata klabu yenyewe ya Yanga imeasisiwa na wazawa wa Dsm ambao wengi wao ni wazaramu

Ni tumaini langu mtasamehe kuuthibitisha uungwana tuliouzoea,

Shukran

Mohamed Bhinda

Mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga.

Arsene Wenger Adhihirisha Kura Yake Kwa Lionel Messi
Baada Ya Marekani Kupitia MCC Kusitisha Msaada Kwa Tanzania, Mbowe Amtaka Rais Magufuli Afanye Haya