Mke wa mchuuzi wa mitaani wa Nigeria Charity Oriachi ambaye mumewe Alika Ogorchukwu aliuawa na Muitaliano Filippo Ferlazzo, ametaka mamlaka zitende haki juu ya kifo cha mumewe kilichozua shutuma kwa baadhi ya mataifa.

Alika Ogorchukwu (39), alikuwa akiuza bidhaa siku ya Ijumaa kwenye barabara kuu ya Civitanova Marche, mji wa ufuo wa bahari ya Adriatic, wakati mshambuliaji wake aliposhika mkongojo wa mchuuzi huyo na kumpiga, kumuangusha kisha kumkaba na kumelekea umauti.

Polisi nchi Italia imesema, “Mshambuliaji ambaye ni mtuhumiwa bwana Ferlazzo alimfukuza mwathiriwa na kwanza kumpiga kwa mkongojo, kisha kumwangusha chini na kisha kummaliza na kumuua kwa kumpiga mara kwa mara kwa mikono yake.”

Baadhi ya watu kutoka jamii ya Nigeria na Italia walikutana kuandamana huko Civitanova Marche kupinga mauaji ya Alika Ogorchukwu nchini Italia. (Picha na The Guardian).

Uchunguzi wa maiti baadaye wiki hii utasaidia kubaini ikiwa Ogorchukwu alikufa kwa kipigo hicho au alinyongwa akiwa amelala na Polisi walitumia kamera za barabarani kufuatilia mienendo ya mshambuliaji huyo na kumshikilia mtuhumiwa Filippo Claudio Giuseppe Ferlazzo (32).

Polisi wameongeza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo mauaji na wizi, baada ya kuchukua simu ya mwathiriwa na kusema mshambulizi alifoka baada ya mchuuzi kufanya maombi kusisitiza kiasi alichohitaji kwa kuwahoji mashahidi na kutazama video za shambulio hilo.

Mwenyekiti wa chama cha Wahamiaji cha ACSIM cha eneo la Marche Mkoa wa Macerata, Daniel Amanza amesema Ogorchukwu alieacha mke na watoto wawili, alianza kuuza bidhaa mtaani baada ya kugongwa na gari na kupoteza kazi yake ya kibarua kutokana na majeraha yake.

Marehemu Alika Ogorchukwu, (39), aliyeuawa katika mtaa mmoja nchini Italia, huku watu wakirekodi shambulio hilo kwenye simu zao bila kuingilia kati na kuzuia mauaji hayo.

Kufuatia tukio hilo, mamia ya watu kutoka jamii ya Nigeria na Italia akiwemo mke wa Orgorchukwu, Charity Oriachi, waliandamana huko Civitanova Marche siku ya Jumamosi kupinga kitendo hicho wakidai kina akisi ubaguzi wa rangi.

Mwanasheria anayewasaidia Wanigeria nchini Italy katika kesi tofauti, Francesco Mantella, amesema, “Hii ni mbaya hakuna anayesaidia kuzuia hasira hii ya mauaji dhidi yake ila kutojali huku na tukio hili la aibu ni lazima lichunguzwe maana inaonyesha kuwa hakuna hisia tena juu ya uraia, usikivu na mshikamano.”

Katibu Mkuu aonya utapeli mtandaoni
Ne-Yo aomba faragha tuhuma za usaliti na Machangudoa