Mke wa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Melania Trump amezua gumzo kubwa kwenye mitandao na vyombo vya habari wakati akitoa hotuba yake kwa wanachama wa chama hicho jana usiku, baada ya kubainika kuwa sehemu kubwa ya hotuba yake amenakili hotuba ya Michelle Obama kwa wanachama wa Democratic mwaka 2008.

Maelezo yaliyoanza kuonekana kwenye vyombo vya habari yalionesha hatua kwa hatua za maneno ya Melania ambazo ni nakala ya maneno ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle.

Hotuba hiyo ilijikita katika kueleza jinsi alivyoingia nchini Marekani pamoja na jinsi anavyompenda mumewe Trump na wanae.

Mapema leo, Melania alimwambia mtangazaji wa NBC, Matt Lauer kuwa aliipitia hotuba hiyo mara moja kwakuwa aliiandika mwenyewe kwa sehemu kubwa ingawa alisaidiana na timu yake.

Michelle na Melania

Kiwanda Cha Pepsi Cha Jijini Dar Es Salaam Chapigwa Faini
Nay Amesema Amewaachia Wanasheria wake Suala la Basata