Tume ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini Congo imetangaza kifo cha mlinda amani ambaye ni raia wa Tanzania.

Kifo hiko kimetokea pindi wakiwa katika mapigano yaliyotokea katika eneo la Beni, kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP tume hiyo imesema kwamba mlinda amani huyo raia wa Tanzania amepigwa risasi wakati wa shambulizi la Jumapili lililofanywa na washukiwa waasi wa kundi la Allied Democratic Forces kwenye eneo la vikosi vya jeshi.

Imesema eneo la jeshi lilikuwa kiasi cha mita 500 kutoka kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa. Tume ya Umoja wa Mataifa imesema mlinda amani mwingine raia wa Tanzania amejeruhiwa katika mapigano hayo na kuwaishwa hospitali ya Umoja wa Mataifa huko Goma.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani mauaji hayo na ameiisihi serikali ya Congo kuchunguza tukio hilo na kuwafikisha waliohusika mbele ya sheria. Katika taarifa yake ameyataka makundi yote yenye silaha nchini Congo kusitisha ghasia.

 

Aliyezuia vita vya nyuklia wakati wa vita baridi afariki dunia
Klopp: Chamberlain anahitaji muda Liverpool