Maafisa wa afya wa Sudan, wamesema takriban watu 26 wamefariki kutokana na homa ya Dengue katika mojawapo ya milipuko mbaya zaidi uliowahi kutopkea katika miaka ya hivi karibuni nchini humo.

Hadi kufikia Jumatatu, Novemba 21, visa 460 vya ugonjwa huo na visa vingine 3,436 vinavyoshukiwa vimerekodiwa, Wizara ya Afya ya Sudan ilitangaza kwenye mitandao ya kijamii.

Takriban vifo 20 vilirekodiwa katika eneo la Kordofan kusini, moja ya maeneo ambayo mlipuko huo uliripotiwa kwa mara ya kwanza na Kamati ya Madaktari wa Sudan mapema mwezi Novemba. Vyombo kadhaa vya habari vya ndani vinaweka idadi rasmi ya kesi kuwa kubwa zaidi.

Homa hiyo ya dengue, ina dalili kama za mafua na mara nyingi inaweza kusababisha kushindwa kwa viungo na kifo ambapo mwaka 2019, Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, lilisema mlipuko wa ugonjwa huo nchini Sudan ulisababisha vifo vya watu watano.

Katika kilele cha msimu wa mvua nchini Sudan mwezi Agosti na Septemba, mafuriko yalisababisha vifo vya takriban watu 144 na kuharibu makumi ya maelfu ya nyumba, pamoja na barabara na miundombinu mingine muhimu.

Hali si shwari KMC FC, Majeruhi waongezeka
Polisi: Hakuna dalili za kupungua kwa uhalifu