Mtu mmoja ameuawa na wengine 14 wamejeruhiwa katika miripuko iliyotokea karibu na vituo vya mabasi mjini Jerusalem.

Polisi katika mji huo, wamesema kuwa wanashuku hilo ni shambulio lililofanywa na Wapalestina huku Shirika la huduma za dharura la Magen, David Adom likisema wanne miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya.

Polisi wakifanya uchunguzi mara baada ya tukio lililosababisha vifo vya watu wawili jijini Jerusalem. Picha ya Sydney Morning Herald.

Tukio hilo, limejiri wakati mivutano ikishamiri baina ya Israel na Wapalestina, kutokana na kuongezeka kwa operesheni za wanajeshi wa Israel katika makaazi ya Wapalestina kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Operesheni hizo ziliimarishwa baada ya wimbi la mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya Israel ambamo watu 19 waliuawa huku Waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu akiwa katika mchakato wa kuunda serikali baada ya ushindi ambao utaipa Israel serikali yenye msimamo mkali.

Tetemeko jingine latokea likijeruhi watu 50
16 wapoteza maisha maporomoko mgodini