Watu 12 wamefariki dunia nchini Nigeria mara baada ya tangi la mafuta kulipuka wakati wakichota mafuta kutoka kwenye tanki hilo lililopasuka na kuvuja mafuta.

Taarifa hiyo imetolewa na polisi waliowasili kwenye tukio hilo pamoja na mashahidi walioshuhudia ajali hiyo.

”Tumepata maiti 12, huku wengine 22 wamejeruhiwa vibaya kwa kuungua na moto na tayari wamefikishwa hospitali kwa matibabu”, Amesema Irene Ugbo msemaji wa polisi.

Amesema mlipuko huo umetokea ijumaa jioni eneo la Odukpani, ambapo ndani ya tanki hilo kulikuwa na watu zaidi ya 60 huku akidai kuwa uwezekano ni mdogo kuwa watu hao wameponea chupuchupu na mlipuko huo.

”Polisi walifanikiwa kupata maiti chache, kwani nyingine tayari ziligeuka majivu” amesema shahidi mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Johnson.

Hata hivyo inasemekana kuwa mlipuko huo umetokana na shoti ya umeme wa genereta lililoletwa katika eneo hilo kusaidia kupampu mafuta kwa ajili ya watu waliokuwa wakiyachota kwenye galoni zao.

Japokuwa bado haijathibitishwa chanzo sahihi cha mlipuko huo.

Aidha, mamia ya watu tayari wamewahi kupoteza maisha katika ajali kama hiyo  miaka michache iliyopita.

Ikiwa mnamo mwaka 1998 kulitokea ajali kubwa kama hiyo ya kulipuka kwa tangi la mafuta na kusababisha vifo vya watu 1000 waliokuwa eneo hilo wakikusanya mafuta hayo.

 

 

Mwalimu anyweshwa sumu na wasiojulikana
Lugola awashukia wanaoponda ujio wa ndege mpya