Jeshi la Togo limesema mlipuko uliotokea kaskazini mwa nchi hiyo umesababisha vifo vya watu saba na watu wawili wamejeruhiwa, ingawa halijafafanua zaidi kuhusu sababu za tukio hilo.

Mlipuko huo ulitokea katika mkoa wa Tone karibu na mpaka na Burkina Faso, ambapo waasi wa Sahel wanatishia kusambaa katika mataifa ya pwani ya Afrika Magharibi.

Togo mwezi uliopita ilitangaza hali ya hatari katika Wilaya zake za kaskazini kutokana na tishio la mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu wa kaskazini mwa mpaka wake.

Askari wakijadiliana jambo Lome, Togo.

Hata hivyo, Jeshi hilo limesema katika taarifa yake kwamba, mlipuko wa Jumamosi katika kijiji cha Margba huko Tone uliua watu saba na wengine wawili kujeruhiwa huku likidai uchunguzi unaendelea.

“Uchunguzi unaendelea ili kubaini mazingira ya mlipuko huu na kubaini wahusika, lakini watu saba wamefariki na wawili wamejeruhiwa” ilisema taarifa ya jeshi hilo.

Haya yanajiri baada ya Wanajeshi wanane wa Togo kuuawa mwezi Mei katika shambulizi kaskazini mwa Togo, karibu na mpaka na wa nchi ya Burkina Faso.

Lango la Hopsitali ya Rufaa ya jijini Lome, Togo

Wanajeshi wa Togo wamepelekwa kaskazini mwa nchi hiyo kujaribu kuzuia vitisho vya wanajihadi wa kusini kutoka nchi za Mali, Burkina Faso na Niger, ambako wanamgambo wenye uhusiano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State wanaendesha harakati zao.

Kocha Zoran Maki kuliboresha Benchi la Ufundi Simba SC
UNFPA:Watu wasizuiwe kuzaana