Polisi nchini Afrika ya Kusini imetoa taarifa ya tukio la hii leo asubuhi Juni 10, 2022 kufuatia kundi la wanaume wasiojulikana wakiwa na bunduki aina ya AK-47 kufyatua risasi kwenye tavern moja eneo la Soweto ambapo sasa idadi ya waliofariki imefikia 15.

Taarifa hiyo ya Polisi iliyolewa na MEC wa Usalama wa Gauteng, Said Faith Mazibuko imesema idadi ya watu waliofariki imeongezeka na kufikia 15 baada ya majira ya saa saba mtu mmoja aliyekuwa mahututi kufariki huku majeruhi 23 waliopigwa risasi nje ya baa ya mji huo wakiendelea na matibabu.

“Tulipigiwa simu mwendo wa saa 12:00 kuwa kuna tukio la mauaji na tuliwasha gari za Polisi haraka, na kwa bahati nzuri tulipata polisi wa eneo lile na tukaungana ili kuwahi kuhudumia eneo la tukio,” amesema.

Maafisa wa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini (SAPS), wakilinda eneo la tulio la mauaji huku wachunguzi wa kiafya wakikagua eneo la uhalifu ambapo watu 14 waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye tavern huko Soweto Julai 10, 2022.

Watu hao, waliokuwa na silaha walifyatua risasi kwenye baa moja majira ya usiku ambapo Shangazi wa mtu mmoja aliyenusurika Zanele Ngcambele, amesema mpwa wake Zama alikuwa msalani wakati risasi zilipoanza kurindima na ikawa ni afadhali kwake.

“Nilijulishwa na binti yangu kwamba kumetokea ufyatulianaji wa risasi kwenye tavern hii na mpwa wangu, Zama alikuwa kwenye tavern sasa alikuwa na bahati kwakweli kwamba hakupigwa risasi maana alikuwa msalani la sivyo asingekuwa hai,” amesema Zanele.

Kiongozi wa kundi lenye itikadi kali la Bunge la Soweto, Nhlanhla Lux Dlamini anasema matukio haya yanazidi kuwa kawaida nchini Afrika Kusini na wapo watu ambao hawashtuki kusikia jambo hilo maana raia wamepiga kelele lakini hali inazidi kuwa tete.

Baadhi ya watu wakiwashuhudia Polisi wanaoendelea na upepelezi katika eneo ambalo watu 15 waliuawa wakati wa tukio la ufyatulianaji wa risasi katika baa moja huko Soweto Julai 10, 2022.

“Inachukiza sana huwezi kuwa na watu 23 wanaopigwa risasi na bunduki za hali ya juu inakuwa ni kawaida sasa hapa Afrika Kusini watu wanazoea na matukio ni mengi sana hii hali inatisha ingawa kuna watu wanaona ni kawaida tu,” alisema Nhlanhla Lux.

Hata hivyo, Polisi katika mji wa Gauteng kwa kushirikiana na wa eneo la Soweto wamesema bado wanaendelea kuwasaka washukiwa hao, ambapo mpaka sasa imesema bado haijajulikana nia hali ya kutekelezwa kwa mauaji hayo.

Polisi wa Soweto wanasema walipofika eneo la tukio, watu 12 walithibitishwa kufariki na wengine 11 walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha lakini watatu walifariki baadaye na hivyo kufanya idadi ya waliofariki kufikia 14.

Serikali kupokea na kutatua kero za umeme
Rais, Waziri Mkuu wathibitisha kuachia ngazi