Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ranil Wickremesinghe wamesema wanalazimika kujiuzulu baada ya waandamanaji kuvamia makazi yao kuwashinikiza wajiuzulu kutokana na madai yao mbalimbali.

Spika wa Bunge la nchi hiyo, Mahinda Yapa Abey amethibitisha kauli za kukubali kwa Viongozi hao kuachia ngazi kwa amani, baada ya waandamanaji kuvamia makazi yao huku wakichoma nyumba ya Waziri Mkuu.

Awali, Waziri Mkuu Wickremesinghe ndiye alitangulia kusema ataachia ngazi baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, ndipo baadaye Spika wa Bunge la nchi hiyo akatangaza kuwa Rais Rajapaksa naye amekubali kujiuzulu kama Wananchi wanavyopendekeza.

Waandamanaji wakijipiga ‘selfie’ ndani ya majengo ya Ikulu jijini Colombo nchini Sri lanka.

Mamia ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, walikusanyika na kuelekea mji mkuu wa wa nchi hiyo Colombo, wakimtaka Rais wao Rajapaksa ajiuzulu baada ya miezi kadhaa ya maandamano yanayopinga usimamizi mbovu wa kiuchumi na hai mbaya ya kimaisha.

Hata hivyo, Rajapaksa atasalia madarakani kwa muda kuhakikisha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani kauli ambayo iliibua shangwe miongoni mwa waandamanaji waliofika katika jiji hilo.

Hata hivyo, katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa katika, ambapo msemaji wa Hospitali kuu ya Colombo alisema watu watatu walikuwa wakitibiwa majeraha ya risasi.

Waandamanaji wakiwa wanaogelea katika ‘swiming pool’ iliyopo Ikulu jijini Colombo, Sri lanka.

Nchi ya Sri Lanka, inakabiliwa na mfumuko wa bei uliosababisha kuagiza vyakula, mafuta na dawa nje kutokana na mzozo wa kiuchumi unaoendelea nchini humo ambao haujawahi kutokea kwa kipindi kirefu.

Mamlaka zinasema baadhi ya waandamanaji (hawapo pichani) walijeruhiwa katika mikusanyiko nchini Sri lanka.

Polisi Soweto yawasaka wauaji, idadi ya waliofariki yaongezeka
Waislamu waaswa kuendeleza upendo na umoja